Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo,(MOI).
Aliyekuwa Mkurugenzi wa MOI, Profesa Abel Makubi, aliteuliwa na Rais Samia, Juni 7 mwaka huu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.