Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, (WHO) Fredros Adhanom Ghebreyesus ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika (WHOAFRO).
Katika ujumbe wake alioutoa kupitia mtandao wa X, Dk Fredros ametoa salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na bunge la Tanzania kufuatia kifo cha Dk Ndugulile ambaye amefariki leo Novemba 27.
Dk Tedros ameandika:
“Nimeshtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha ghafla cha Dkt Faustine Ndugulile, @WHOAFRO
Mkurugenzi Mteule wa WHO Afrika. Salamu zangu za rambirambi ziende kwa familia yake, marafiki zake, bunge na watu wa Tanzania.”