Idadi ya watu waliofariki baada ya jengo la ghorofa kuanguka Novemba 16 eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, imefikia watu 29.
Hayo yameelezwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, akizungumza na vyombo vya habari akiwa eneo la Kariakoo na kueleza kuwa miili mingine 19 imepatikana katika harakati za uokoaji zilizokuwa zikiendelea katika jengo hilo.
Novemba 22 mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema idadi ya vifo imefikia 16.
Kuhusu mmiliki wa jengo lililoporomoka, ambaye Rais aliagiza ahojiwe, Makoba amesema:
“ Mwenye jengo hili hawezi kukosa kujulikana, tunamjua na mmoja wao ameshatiwa nguvuni ) kwa kwa sababu ni suala la kiuchunguzi Polisi wakiwa tayari watatoa taarifa ili tusiharibu uchunguzi, na niwahakikishie tu Watanzania Serikali haiwezi kushindwa kwahiyo tuwe na amani na majibu yatapatikana”
Kadhalika Makoba amesema, wamiliki hao ni wawili na mmoja tayari ameshakamtwa na hivyo akawataka wananchi wawe na amani na waiache serikali ifanye kazi yake hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
Jengo hilo la ghorofa lililopo eneo la Kariakoo, Ilala, jijini hapa liliporomoka Novemba 16 saa 2 asubuhi na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa na vifo 29.