Msafara wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, umekamatwa na jeshi la polisi eneo la Halungu, wilaya ya Mbozi, Mbeya.
Mbowe akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, na Mwanaharakati wa CHADEMA, Mdude Nyagali, maarufu Mdude Chadema walikamatwa mara tu baada ya kumaliza kampeni katika kata ya Itaka, eneo la Halungu.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, imeeleza:
“Kabla ya kuwakamata walifuatwa na gari ya Polisi ambayo ilikutana nao njiani na hivyo iligeuza na baada ya mwendo kidogo walikuwa njia imefungwa na gari za polisi ndipo walipofungua milango Kwa nguvu na kuanza kuwashambulia waliokuwa kwenye Magari hayo na kuwakamata Kwa nguvu,” I mesema taarifa hiyo
Wengine waliokamatwa ni Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo, Wilaya ya Mbozi na Mbunge mstaafu wa Mbozi(CHADEMA)Paschal Haongo na wafanyakazi wengine wa chama hicho.
“Jeshi la Polisi wameondoka na viongozi wetu na hajajasema wanawapeleka wapi na mpaka Sasa hatujui wanashikiliwa wapi na Kwa sababu gani” imesema taarifa hiyo
Chadema katika taarifa yake kimelaani kitendo hicho na kuzialika jumuiya za kimataifa, kushuhudia uvunjifu wa haki za kidemokrasia kwa vyama vya siasa nchini.