Saa chache baada ya video inayomuonyesha mfanyabiashara Deogratius Tarimo, mkazi wa Kiluvya Kibaha,akisukumwa kwa nguvu na kulazimishwa kuingia kwenye gari na watu wasiojulikana, Wakili wa Kujitegemea, Jebra Kambole ametaja hatua tano za tahadhari za kuchukua iwapo utakutana na tukio linalofanana na la Tarimo.
Kambole ameandika katika ukurasa wake wa X, akisema:
Usikubali kukamatwa na mtu;
1. Kavaa kiraia
2. Gari halina No. au No za kiraia
3. Watu ambao hawajatoa vitambulisho
4. Watu wasiokwambia kosa lako na kwamba uko chini ya ulinzi.
5. Watu wasio na hati ya ukamataji!