Katibu wa CCM, wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, Christina Kibiki, ameuawa kwa kupigwa risasi leo wilayani Kilolo, Iringa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makala leo, imeeleza kabla mauti hayajamfika, Kibiki alikuwa akijiandaa kwa safari ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya semina ya makatibu wa chama, inayotarajiwa kufanyika kesho.
“Tunawaomba wanachama wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia ili wahusika wafikishwe katika vyombo vya sheria”imesema sehemu ya taarifa hiyo.