Wino Ripota
Dhana kuhusu hedhi salama ni jambo kubwa katika jamii nyingi hapa Tanzania.
Wapo wanaosema, mwanamke aliye katika hedhi, haruhusiwi kuchuma mboga au kushika mimea, kwani itanyauka.
Wapo wanaosema, mwanamke aliye katika hedhi hatakiwi kushiriki shughuli zozote za uvuvi au uchimbaji wa madini kwa sababu atasa abisha nuksi.
Wapo wanaosema, mwanamke aliye katika hedhi, hatakiwi kutoka nje kwa sababu ni najisi.
Lakini haya yote ni dhana potofu na ni ukosefu wa elimu sahihi kuhusu hedhi salama.
Taasisi ya TAI Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataif la kuhudumia Watoto (UNICEF) wameunda program maalum inayowasaidia Watoto wa kike kupata taarifa sahihi kuhusu masuala ya afya ya uzazi, ikiwamo hedhi salama.
TAI, walibuni program hiyo ya OKY, ‘kutoka kwa binti, kwenda kwa binti’ inayowawezesha Watoto wa kike kujua tarehe ya kupata hedhi ijayo, dalili za kupata hedhi na taarifa sahihi kuhusu hedhi.
Akizungumza katika kongamano la kimataifa la kuimarisha ubora wa elimu(IQEC)Meneja Miradi (TAI) Mariam Mintanga amesema waliangalia na kubaini changamoto kubwa iliyopo ni ukosekanaji wa taarifa sahihi za afya ya uzazi kwa Watoto wa kike.
“Hawafundishiw shuleni wala nyumbani, matokeo yake, wanakosa taarifa sahihi, kwa hiyo ‘app’ hii itawapa taarifa sahihi kuhusu hedhi, mzunguko, dalili na ukweli kuhusu hedhi,” amsema Mitana
Amesema kadhalika program hiyo katika kipengele cha maktaba inatoa elimu kuhusu dhana na ukweli kuhusu hedhi.
“Kuna baadhi ya mila zinasema, mwanamke akiwa kwenye hedhi hafai kuchuma mboga, hatakiwi kupika au hatakiwi kushiriki shughuli fulani, wakati sio kweli. Sasa ‘app’ hii inaweka wazi kuhusu dhana na ukweli,” amesema
Pamoja na taarifa za hedhi lakini pia, Mariam anasema binti anaweza kupata taarifa kuhusu ukatili wa kijinsia na hatua anazopaswa kuchukua endapo atafanyiwa ukatili.