Balthazar Ebang Engonga, amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii tangu Novemba 4, baada ya video za ngono kuvuja zikimuonyesha akifanya vitendo vya ngono na wanawake tofauti.
Lakini je unamjua Ebang ni nani?
Balthazar Ebang Engonga ni msomi mwenye utaalamu katika fani ya Uchumi. Alipata shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Malabo, Equatorial Guinea.
Amewahi kufanya kazi kama mhasibu katika kampuni ya uchimbaji nchini humo. Baadaye, alipata ajira katika kitengo cha serikali nchini humo cha GEPROYECTOS ambacho huundwa na rais kwa ajili ya kusimamia, kudhibiti miradi mikubwa ya taifa.
Baadaye, Balthazar alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi na Usimamizi wa Fedha nchini humo.
Baba yake Balthazar, Edjo Engongo aliwahi kwua Waziri wa Uchumi nchini humo, na sasa ni Rais wa Tume ya Uchumi na Jumuiya za Kifedha Afrika ya Kati(CEMAC).
Balthazar, ana mke na watoto sita.