Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha (ANIF) Equatorial Guinea.
Engonga amezua taharuki baada ya video zaidi ya 300 kubainika kazika kompyuta ya ofisini kwake, zikimuonyesha akifanya ngono na wanawake tofauti tofauti akiwamo mke wa kaka yake na dada wa Rais wa nchi hiyo.
Engonga, ambaye ana mke na watoto sita, ni mfanyakazi wa serikali na mtaalamu wa masuala ya intelijensia ya fedha katika ofisi ya Waziri wa Fedha nchini humo.
Miongoni mwa wanawake wanaodaiwa kuonekana wakifanya vitendo vya ngono na Engonga ni pamoja na mke wa kaka yake, wafanyakazi wenzake wa wizarani na dada wa Rais wa Equatorial Guinea.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, wanawake waliorekodiwa katika video hizo walikubali kwa hiyari yao.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Nguema ametangaza kuwasimamisha kazi wafanyakazi wote wa serikali walioonekana katika video hizi zilizosambaa mitandaoni kuanzia jana.