Duma Boko, Mwanasheria, Mwalimu wa Sheria na baba wa Watoto tisa, anatajwa kuwa ndicho chanzo cha mapinduzi makubwa nchini Botswana, baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana na kukitoa chama cha upinzani madarakani.
Chama Kikuu cha upinzani, Umbrella for Democratic Change (UDC), kimeongoza kwa idadi ya kura, katika matokeo ya awali, ambapo Duma Boko, anaongoza kwa kura hali inayoonyesha wazi kuwa ushindi wa Duma unawaleta wapinzani kama chama tawala baada ya BDP kukaa madarakani kwa miaka 58, tangu nchi hiyo ipate uhuru.
Boko, mwenye umri wa miaka 54, alianzisha chama cha UDC, mwaka 2012 na kuunganisha vyama vya upinzani ili kukitoa madarakani BDP. Hii ni mara yake ya tatu kuwania urais, kuanzia mwaka 2018.
Kaone Boko, mke wa Duma, alifunga ndoa na rais huyo mtarajiwa mwaka 2013. Kaone anatajwa na jarida la Botswana Herald kuwa ni mwanasheria kitaaluma.
Kaone, amekuwa ni msimamizi mkuu wa kampuni ya sheria ya Duma, lakini pia amekuwa akishiriki kwa kiasi kikubwa shughuli za kisiasa na kampeni za urais za mume wake.Kaone, alifunga ndoa na Duma, mwaka 2013,
Zandile Boko, shangazi wa Duma, anamzungumzia, Duma akiwa kijana mdogo, na kumtaja kama mtulivu na mfadhili wake mkubwa.
“Yeye na mke wake wananilisha na kunitunza. Ananipenda kwa dhati.” Anasema na kumtaja Duma kama mtu mvumilivu
Zandile anasema, alipata wasiwasi wakati Duma alipoingia katika siasa, na kusema:
“Watu hawana upendo tena, na ni mbaya zaidi katika siasa. “
- Duma Boko (54) amezaliwa Desemba 31, 19689 mji wa Mahalapye, Botswana.
- Duma ni mwanasheria na amekuwa mwalimu wa sheria kuanzia mwaka 1993 hadi 2003 alipokimbilia kwenye siasa.
- Boko ndiye aliyeanzisha umoja huo wa vyama vya upinzani mwaka 2012.
- Amewahi kuwa kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, 2014 hadi 2019.
- Mke wa Duma, ni Kaone Boko na wana Watoto 9
- Amesoma elimu ya juu ya Sheria Chuo Kikuu cha Botswana na Havard, Uingereza.
MASISI AMEKIRI KUSHINDWA
Rais wa Botswana, Mokgweetis Masisi, amekubali kushindwa katika matokeo ya awali ya uchaguzi huo, ambayo yanaonyesha kuwa chama tawala kimepoteza viti vingi vya ubunge baada ya kuwepo kwa miongo sita madarakani.
Rais Maasisi, amekubali kushindwa katika uchaguzi huo kabla hata matokeo hayajatangazwa, ambapo chama chake Democratic Party, (BDP) kikishinika nafasi ya 4 baada ya matokeo ya awali kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo.
‘Tumekosea vikubwa mbele ya macho ya watu” Masisi amewaambia wanahabari katika mkutano uliofanyika mji mkuu wa Gaborone, Botswana
Rais Masisi, alikuwa akisaka msimu wake wa pili wa miaka mitano wa uongozi, alikiri, kushindwa na kuachia Madaraka.
Boko ameandika katika ukurasa wake wa Facebook leo asubuhi akisema;
“Mabadiliko haya hapa”