Siku hizi msamiati wa lugha ya kiingereza, usemao;’delivery’ umekuwa maarufu na neno hilo lina maana ya kufikisha.
Sasa basi, kama hukuwahi kusikia, basi sikia hii: Chakula aina ya pizza, kiliwahi kufikishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro eneo ambalo ni meta 5897 na urefu wa futi 19,347.
Tukio la kufikishwa kwa pizza hii katika mlima Kilimanjaro, limevunja rekodi ya Guinnes ya kufikisha Pizza katika umbali huo.
Pizza hiyo ilifikishwa Mei 5-8 mwaka 2016 wakati wa uzinduzi wa duka la kwanza la kuuza Pizza Tanzania(Pizza Hut).
Kampuni ya Pizza Hut ya Afrika Kusini, kwa kushirikiana na Yum!Brand (USA) walifikisha pizza hiyo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro tukio ambalo lilivunja rekodi ya Guiness ya kufikisha Pizza umbali huo.