
Tanzania imethibitishwa kuwa na wagonjwa wawili wenye virusi vya homa ya nyani au Mpox.
Mara baada ya serikali kuthibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo, wataalamu wa afya wameeleza namna virusi hivyo vinavyoweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Daktari Bingwa wa Mgonjwa way Mifupa na Maungio(Rheumatologist) na mhariri mkuu wa jarida la Afya la Havard, Robert H. Shmerling amefafanua namna maambukizi ya Mpox yanavyoweza kutokea.
Moja ya sababu zinzotajwa kuchagiza kuenea kwa ugonjwa wa MPOX kwa mujibu wa Dk Shmerling ni wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani(WHO) Septemba mwaka jana imeeleza kuwa, virus vya Mpox huweza kumdhuru yeyote lakini kwa mujibu wa kesi zinazoripotiwa kwa wingi ni za wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na watu wenye mpenzi zaidi ya mmoja wapo hatarini zaidi. https://www.who.int/news-room/public-advice/men-who-have-sex-with-men-preventing-monkeypox
USIYOYAJUA KUHUSU MPOX
HOMA YA NYANI NI UGONJWA GANI?
- Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya jamii ya ndui(smallpox) ambao awali ulitajwa kuanzia magharibi mwa Afrika, na kusambazwa zaidi na Wanyama kama kicheche na panya.
DALILI
- Mafua makali
- Homa
- Kichwa kuuma
- Kuvimba kwa tezi za mwili
- Vipele vikubwa na vigumu visivyotumbulika
- Vipele hivyo hukaa kwa wiki mbili na kuwa uvimbe mdogo wenye majimaji kama tete kuwanga na baadaye kuwa vikubwa kama malengelenge
- Baada ya muda , malengelenge hayo hukauka na kupona
MAAMBUKIZI
- Kushikana na mtu mwenye maambukizi au mnyama
- Kushika nguo au vifaa au eneo ambalo limeshikwa na mtu mwenye virusi hivyo
- Kuishi kayika maeneo au kutembelea miji ambako virusi vya mpox vimesambaa
- Wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja
- Kuwa na wapenzi wengi