
Wino Tanzania
Mwasisi wa asasi za kimaendeleo duniani za Aga Khan na Karim Al-Hussaini, Aga Khan wa IV amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, akiwa na umri wa miaka 88.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika tovuti ya Aga Khan, Prince Hussaini amefariki dunia huko nyumbani kwake Lisbon,Portugal jana Februari 4.
Prince Karim Aga Khan alikuwa ndio mwanzilishi na mwenyekiti wa mtandao wa maendeleo wa Aga Khan ikiwamo hospitali, hoteli, miradi ya maendeleo ya elimu na Watoto.
Aga Khan kabla ya umauti alikuwa ni kiongozi wa kidini wa watu zaidi ya milioni 12, wa dini ya kiislamu, uongozi ambao aliurithi akiwa na umri wa miaka 20.
Kwa hapa Tanzania, Aga Khan ina miradi ya maendeleo ikiwamo ya Afya,(Aga Khan Hospital), Elimu(Aga Khan Schools and Universities), Uchumi(Hoteli za Serena), Kilimo na Vyombo vya habari.

Al-Hussaini alikuwa ni Imamu wa dini ya Shia akiwa na umri wa miaka 20 na ana utajiri wa zaidi ya euro 11 bilioni.
Aga Khan, alikuwa ni rafiki wa karibu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza na mtoto wa Malkia huyo, Prince Charles.