
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John John Mnyika akizungumza na wanahabari leo.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John John Mnyika, amewapa onyo wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho na kuwataka wafuate kanuni, maadili na miongozo ya chama hicho wakati wa kampeni.
Mnyika ameyasema hayo leo, Januari 7th wakati akizungumza na wanahabari na kutoa mrejesho wa idadi ya waliochukua fomu za kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama.
“Ninawataka wanaowania uongozi kuzingatia miongozo, kanuni na maadili, hasa miongozo ya rushwa na kuepuka kampeni zinazojikita katika udini, ukabila na ukanda,” amesema Mnyika
Kuhudu idadi ya wagombea, Mnyika amesema, jumla ya waliochukua fomu kuwania uongozi ndani ya Baraza la Wazee Chadema, Baraza la Vijana Chadema, Baraza la Wanawake Chadema, ni 300.