
Waziri Dorothy Gwajima, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Wakati mitandao ya kijamii ikiendelea kuwa chombo kikuu cha mawasiliano na utoaji taarifa,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dk Dorothy Gwajima amewaonya watengeneza maudhui mitandaoni(online content creators,) akiwataka kuacha kutuma maudhui yanayodhalilisha, yanayochagiza ukatili wa kijinsia na yanayokwenda kinyume na miongozo ya kisera na sheria.
Katika taarifa yake aliyoitoa leo Januari 6, Dk Gwajima ametoa mifano ikiwamo maudhui kijana aliyebeba mtoto na kutangaza kuuza figo yake.
“Natoa wito kwa waandaa maudhui wote kuzingatia weledi na miongozo, kama mtu hana elimu na ufahamu, kuhusu kuandaa maudhui mitandaoni, aache mara moja maana ataharibu na atawajibishwa” Gwajima amesema Kadhalika Waziri Gwajima ameagiza, kwa wale walioweka maudhui kinyume na miongozo husika, wayaondoe mara moja