Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na treni ya kisasa ya SGR wamekwama baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.
Baadhi ya abiria waliokuwa katika treni hiyo wamesema imekwama kwa saa kadhaa sasa.
Inaelezwa kuwa treni hiyo imekwama stesheni ya Kilosa, Morogoro.
“Tuko hapa tunasubiri umeme urudi ndio safari iendelee, tumeambiwa Grid ya Taifa imezima..”kimesema chanzo cha habari, ambaye ni abiria katika treni hiyo.
Hata hivyo, taarifa ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeeleza kuwa kumetokea hitilafu kwenye gridi ya Taifa hivyo kusababisha umeme kukatika kwenye baadhi ya mikoa inayohudumiwa na gridi ya Taifa