Mwenyekiti wa Chadema, Kitongoji cha Muyaga ‘C’, ijiji cha Kitahana, kata ya Kitahana, Wilaya ya Kibondo Onesmo Saimoni Mdollo ameokotwa leo Desemba 4 asubuhi akiwa na majeraha mbalimbali mwilini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA, Onesmo, wakati anaokotwa alikuwa hajitambui na alishindwa kuzungumza chochote.
“mwili wake umekutwa na majeraha. Onesmo amekutwa barabarani, jirani na shule ya msingi Kabwigwa” imesema taarifa hiyo.