
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema lugha inayotumika sasa ya ‘uchawa’ inawaaminisha wananchi kwamba mtu mmoja anaweza kufanya kila kitu au kwa maana nyingine amesema inakaribisha udikteta.
Jaji Warioba ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali ikiwamo uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika.
“Tunajua serikali inavyofanya kazi, tunajua ni uongozi jumuishi. Lakini sasa tuna lugha, tunataka wananchi waamini kwamba kuwa ni mtu mmoja, anaweza kufanyakila kitu,” amesema na kuongeza:
“Ndiyo naogopa, maana inawezekana itafika siku tukamchagua mtu ambaye anataka kiwa dikteta. Ingawa Rais mwenyewe wa sasa haonyeshi ‘tendency’ ya udikteta”
Jaji Warioba amesema, uchawa ni dalili ya kukaribisha udikteta na kwamba anaachiwa mtu mmoja na akashauri, demokrasia iimarishwe na vyama vya siasa viimarishwe.