Mgombea wa nafasi ya ujumbe kata ya Gongolamboto, Mtaa wa Ulongoni, Modestus Timbisimilwa, ameuawa leo mchana baada ya kupigwa.
Chadema wametoa taarifa hiyo katika mtandao wao wa X, na kueleza kuwa, Modestus amefariki mchana huu baada ya kupokea kipigo kutoka kwa jeshi la Polisi, wakati akizuia kura feki kuingizwa kwenye sanduku la kura.