Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Kitongoji, cha Stand, kata ya Mkwese, Jimbo la Manyoni, Mashariki kupitia CHADEMA, George Mohamed ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA kupitia mtandao wa X leo, George alivamiwa na watu wasiofahamika hali iliyosababisha mzozo na baadaye polisi walifika nyumbani kwake na kumpira risasi kiunoni.
Katika tukio jingine CHADEMA kimesema, kiongozi wa chama hicho eneo la Tunduma, Steven Chalamila ameuawa baada ya kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.