
Wino Ripota
Jeshi la polisi Tanzania linawashikilia na kuwahoji wafanyabiashara wawili, Diva Gissele Malinzi, maarufu Diva mkazi wa Mikocheni, na Jennifer Jovin Bilikwija maarufu Niffer mkazi wa Salasala kwa tuhuma za kukusanya pesa kwa kutumia akaunti zao binafsi wakidai wanakusanya michango kufuatia janga la kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro,imeeleza kuwa, Jennifer, Maarufu Niffer, amekatwa Dodoma na amerejeshwa Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.

Kadhalika taarifa hiyo imesema jeshi hilo litashirikiana na mamlaka zingine kisheria kuona hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.
“Jeshi la polisi linaendelea kutoa tahadhari na halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au watu ambao yanapotokea matatizo au majanga, wao huona ni fursa ya kujinufaisha” imesema taarifa hiyo iliyotolewa leo Novemba 19.