Wino Ripota
Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, iliyopangwa kufanyika nchini Cuba kuanzia Novemba 6 hadi 8, imeahirishwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ziara hiyo imeahirishwa baada ya serikali ya Cuba kutangaza kuwepo kwa kimbunga Rafael kuanzia Novemba 6 hadi 7. Kutokana na kimbunga hicho, serikali ya Cuba imezuia safari za ndege zinazoingia na kutoka.
Badala yake, Rais amewaagiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Damas Ndumbaro kuratibu shughuli zilizopangwa kufanyika wakati wa ziara hiyo.