
DUNIA inasubiria kwa hamu kuona ni supastaa gani ataibuka kinara na kubeba tuzo ya Ballon d’Or 2024. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika leo usiku Oktoba 28, 2024 jijini Paris, Ufaransa.
Hata hivyo, kwa mara ya tatu tangu mwaka 2007, tuzo hiyo kubwa kwa wanasoka duniani itakwenda kwa mchezaji tofauti nje ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo baada ya mastaa hao kutawala kwa kubadilisha kila mwaka.
Kwa mwaka huu orodha ya wanaowania tuzo hiyo haitakuwa na jina la Ronaldo wala Messi kama ilivyozoeleka miaka kadhaa iliyopita.

Hata hivyo, taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari nchini Uingereza, zinaeleza kuwa staa wa Real Madrid forward, Vinicius Junior ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuibeba usiku huu. Mbali na Vinicius mwenye alama 630 akifuatiwa na kiungo wa Manchester City, Rodri anayeshika nafasi ya pili.
Mbali na Vinicius na Rodri, wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham akiwa nafasi ya tatu. Wengine ni Harry Kane (England-Bayern Munich), Erling Haaland (Norway-Manchester City), Phil Foden (England-Manchester City), Kylian Mbappe (Ufaransa- Real Madrid) na Lamine Yamal (Hispania-Barcelona).
Pia wamo Dani Olmo (Hispania-Barcelona), Florian Wirtz (Ujerumani-Bayern Leverkusen), Dani Carvajal (Hispania-Real Madrid) na Antonio Rudiger (Ujerumani-Real Madrid).